MAISHA YA CHUONI, TAMATI NIMEFIKA
Kumbukizi za kujiunga na Chuo Kikuu cha Kiufundi cha Mombasa almaarufu Technical University of Mombasa,bado zimo akilini mwangu.Siku hiyo ya kujiunga na Chuo hiki ilikuwa Jumatatu ya tarehe ishirini na tano ya mwezi Januari mwaka wa elfu mbili ishirini na moja masaa ya asubuhi.Hapo awali nilikuwa nimepata mwaliko wa kujiunga na Chuo hiki kusomea taaluma ya habari na Mawasiliano.Ni ndoto ambayo nilitamani Sana siku moja kuwa mwanahabri tajika kama Rashid Abdhalah wa runinga ya Citizen.Siku hiyo nilivalia suti ya rangi nyeusi tititi na shati leupe pepepe kama maziwa huku likiwa limepigwa pasi kiasi ya kwamba nzi angetua juu ya shati hilo basi angefariki papo hapo. Nilifika katika afisi za usajili wa wawanagenzi,nikakabidhiwa barua ya usajili kisha nikaamuriwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi.Kwa kuwa ilikuwa siku yangu ya kwanza kukanyaga chuo hicho,sikuwa na budi ila kuomba msaada wa kuelekezwa jinsi ya kujaza fomu hiyo.Kulitokea janadume ila lilinipea masharti ambayo sikuweza kuyaep...