MACHO YOTE
SASA YAELEKEZWA KWA VIJANA KATIKA KUFUFUA UCHUMI WA TAIFA
Je, vijana wana umuhimu wowote katika kufufua uchumi wa Kenya? Hilo ndilo swali ambalo linazidi kuumiza mishipa vichwani mwa waja wengi katika siku za hivi sasa.Hali ya uchumi imeenda juu kiasi kwamba imekuwa donda sugu lisilopona.Mamia ya waja wanazidi kupoteza maisha yao kila uchao kutokana na njaa ambayo imesababishwa na gharama ya juu ya maisha.Familia nyingi haziwezi kujimudu tena sikwambii kutosheleza mahitaji yao ya kimsingi.Habari zinazongonga vichwa vya wanahabari kila uchao ni kwamba suluhu itapatikana wapi ili kuokoa maisha ya binadamu?Wanahabari kote nchini wapo ange kuhakikisha kuwa wanataoa taarifa kemkem kuhusu familia zilizoathirika kutokana na kupanda kwa uchumi hapa nchini.Ni lazima kama ibada kuwa kilicho na sifa acha kipewe sifa, hii ni kumaanisha kuwa hongera kwa wanahabari wetu waliosimama kidete na kuangazia masaibu ya waja wanayopitia,ni kutokana na bidii zao za kuripoti ndiposa wahisani kutoka kila pembe ya nchi wamejitokeza waziwazi kama jino la ngiri na kusaidia waathirika.
Hayo yote tisa, kumi ni kuwa vijana pia wana uwezo mkubwa
katika kurudisha sura mpya ya taifa la Kenya jinsi lilivyokuwa hapo awali.Kusema
kweli hali ilivyo sasa inahuzunisha na kustaajabisha mno.Bei za bidhaa muhimu
ziko juu kama bendera lakini matumaini yangalipo kwani vijana wako mbioni
kuhakikisha kila kitu kinarudi pahali pake.Kwanza kabisa vijana wako mbioni
kutafuta vibaraua ili kukidhi mahitaji ya yao ya kimsingi, ni kupitia ajira
hizo ndio uchumi wa taifa letu utafufuka.Hongera kwa serikali kwa kuwa na mpango wa kupatia vijana mtaji ili waanzishe biashara.
Fauka ya hayo,vijana wanapojihusisha na ajira bila shaka
watalipa ushuru kama ilivyo ada na desturi katika taifa letu tukufu la Kenya,
kutokana na hiyo pesa ya ushuru ndipo serikali itaweza kupanga mipango kabambe
ya kuamsha hali ya uchumi iliyolala fofofo.Pia vijana watafufua uchumi wa taifa
pindi watakapojihusisha na mambo na kilimo ikizingatiwa kuwa kilimo ndio uti wa
mgongo wa Kenya.Vijana endapo watajitolea asilimia mia kwa mia na kuzamia
kilimo basi nchi yetu itaweza kuzalisha chakula kwa wingi na janga hili la njaa
tutalizika katika kaburi la sahau.Tukizingatia kilimo basi taifa hili litaweza
kutosheleza waja wake na hata kuuza bidhaa zetu mataifa ya nje na hapo ndipo
tutapata pesa zaidi ya kustawisha Kenya yetu.Vijana tusilalie masikio tujitume
katika ukulima ili tuweze kujitegemea wenyewe siku za usoni.Pia tukiweza
kujitegemea serikali yetu itapumua katika kuomba mikopo kutoka mataifa mengine.
Mbali na hayo ni kwamba kubuniwa kwa nafasi za kazi kwa vijana na serikali za kaunti na kitaifa kutawezesha vijana kuinua uchumi wa taifa uliodorora kwa siku nyingi.Vile vile vijana wanao uwezo wa wao binafsi kujifungulia biashara na hali hii itachangia kurudisha hali ya uchumi ilivyokuwa hapo awali.Pindi vijana wanapojiingiza kazini basi visa vya utovu wa usalama pia vitapungua mara dufu.Hali ya usalama itarudi kama kawa kama dawa kwa sababu kila mmoja atakuwa anatosheka na pato lake.Hata hivyo pindi vijana watakaporudisha hali ya uchumi pahali pake basi wageni wengi watazuru taifa letu na kutokana na hilo tutapata pesa za kigeni ambazo zitatumika katika kueka muonekano mpya wa taifa letu.Kilicho na mwanzo hakikosi mwisho,wito kwa serikali yetu ya kitaifa kuhakikisha swala la ajira kwa vijana inalipa kipaumbele kwani vijana ndio kioo cha jamii.Vijana kama ilivyo ada na desturi kuwa nyinyi ndio tegemeo la siku za usoni basi hatuna budi kung’ang’ana kama mchwa kichuguuni ili kuboresha na kurudisha hali ya uchumi wa taifa la Kenya mahali ulipokuwa.
Mwandishi wa Makala haya ni Mohammed Kazungu kutoka Chuo kikuu cha Kiufundi cha Mombasa (TUM)


Heko
ReplyDeleteKazi mbashara umegonga ndipo
Big up man, kazi safi
DeleteHongera bro kazi Safi unafanya
DeleteShabash💯
DeleteKongole moha
DeleteAmezing brother
DeleteKazi safi.
ReplyDeleteKazii nzuri
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteHuu ndio Wimbo kila sehemu ya Dunia.Jitahidi sana kujiajiri tuepuke hili
ReplyDeleteAmina Masha
ReplyDeleteHeko
DeleteHongera sana
DeleteKongole kaka Kwa kazi iliyo njema
DeleteNakala Safii
ReplyDeletegood job
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteSafiii
ReplyDeleteKazii safi
ReplyDeleteSwadakta
ReplyDeleteNice and good
ReplyDelete👌👌👌👌
ReplyDeleteGood one
ReplyDeleteMzuri sana
ReplyDeleteKazı safi
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteGood
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteHongera kaka✍️✍️🔥
ReplyDeleteSadakta
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteWell done
ReplyDeletekazi safi
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteBig ups bro
ReplyDeleteGreat
ReplyDeleteGood job
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteNice One 👌
ReplyDeletekazi nzuri
ReplyDeleteNoma sanaaa
ReplyDeletePongezi
ReplyDeleteTop
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteAsantaaa
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteNice piece
ReplyDeleteKazi nzuri 👏👏
ReplyDeleteNzuri sana kaka
ReplyDeleteKweli kabisa
ReplyDeleteKazi safi kaka
Swadakta,
ReplyDeleteNakala nzuri
ReplyDeleteNakupa kongole
ReplyDeleteUmeandika vizuri
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteNakala nzuri
ReplyDeleteUko juu brother nice one
ReplyDeleteStreaming article
ReplyDeleteHeko kaka
ReplyDeleteNice one
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteHeko 👏
ReplyDeleteAnother beautiful narration, keep it up buddy
ReplyDeleteGood job
ReplyDelete