Posts

Showing posts from November, 2022

MAISHA YA CHUONI, TAMATI NIMEFIKA

 Kumbukizi za kujiunga na Chuo Kikuu cha Kiufundi cha Mombasa almaarufu Technical University of Mombasa,bado zimo akilini mwangu.Siku hiyo ya kujiunga na Chuo hiki ilikuwa Jumatatu ya tarehe ishirini na tano ya mwezi Januari mwaka wa elfu mbili ishirini na moja masaa ya asubuhi.Hapo awali nilikuwa nimepata mwaliko wa kujiunga na Chuo hiki kusomea taaluma ya habari na Mawasiliano.Ni ndoto ambayo nilitamani Sana siku moja kuwa mwanahabri tajika kama Rashid Abdhalah wa runinga ya Citizen.Siku hiyo nilivalia suti ya rangi nyeusi tititi na shati leupe pepepe kama maziwa huku likiwa limepigwa pasi kiasi ya kwamba nzi angetua juu ya shati hilo basi angefariki papo hapo. Nilifika katika afisi za usajili wa wawanagenzi,nikakabidhiwa barua ya usajili kisha nikaamuriwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi.Kwa kuwa ilikuwa siku yangu ya kwanza kukanyaga chuo hicho,sikuwa na budi ila kuomba msaada wa kuelekezwa jinsi ya kujaza fomu hiyo.Kulitokea janadume ila lilinipea masharti ambayo sikuweza kuyaep...
Image
  MACHO YOTE SASA YAELEKEZWA KWA VIJANA KATIKA KUFUFUA UCHUMI WA TAIFA                 Picha angavu kwa hisani ya Google Je, vijana wana umuhimu wowote katika kufufua uchumi wa Kenya? Hilo ndilo swali ambalo linazidi kuumiza mishipa vichwani mwa waja wengi katika siku za hivi sasa.Hali ya uchumi imeenda juu kiasi kwamba imekuwa donda sugu lisilopona.Mamia ya waja wanazidi kupoteza maisha yao kila uchao kutokana na njaa ambayo imesababishwa na gharama ya juu ya maisha.Familia nyingi haziwezi kujimudu tena sikwambii kutosheleza mahitaji yao ya kimsingi.Habari zinazongonga vichwa vya wanahabari kila uchao ni kwamba suluhu itapatikana wapi ili kuokoa maisha ya binadamu?Wanahabari kote nchini wapo ange kuhakikisha kuwa wanataoa taarifa kemkem kuhusu familia zilizoathirika kutokana na kupanda kwa uchumi hapa nchini.Ni lazima kama ibada kuwa kilicho na sifa acha kipewe sifa, hii ni kumaanisha kuwa hongera kwa wanahabari wetu waliosimama kidete na ...