MABADILIKO YA HALI YA ANGA, MAJONZI KWA BINADAMU
Labda nikisema dalili za kiama zimeanza kuonekana nitazidi kuumiza mitima ya waja hapa duniani, ila kusema ukweli ni kwamba watu wanazidi kuumia na kuteseka kila uchao kutokana na mabadiliko ya ghafla ya hali ya anga.Ni mara ngapi tumesikia vifo vya watu kutokana na makali ya njaa ambayo yamechangiwa na tabianchi? Hapo awali enzi za babu za babu zetu mambo yalikuwa nywee! Yani asili hizo maisha yalikuwa matamu kama asali sikwambii halua, watu wa jadi hizo waliishi maisha ya raha na starehe huku wasijue bei ya vyakula ni nini.Maisha yao yalikuwa shwari kama ya peponi ila sasa,ni vilio na simanzi kila pembe ya taifa letu tukufu la Kenya. Walumbi husema,msiba wa kujitakia hauna kilio lakini huu wa sasa uko na kilio kikubwa sana.Kila jambo mtu analonuia kulifanya ni lazima kama ibada kukadiria matokeo yake yatakuwaje kabla kuamua kulifanya.Shida nyingi tunazopitia tumezichangia sisi wenyewe,tumekumbatia kikiki mfumo mpya wa kitekinolojia ambao umetuathiri sisi binafsi vibaya. Jambo la...