HALUWA SI TAMU TENA VYUONI
Ukishikwa shikamana
Nakubaliana na wasanii asilimia mia kwa mia walipoimba kuwa mapenzi ya siku hizi ni ''COME WE STAY'.Mapenzi ya siku hizi yamegeuka na vilio kila pembe ya dunia.Vile vile kumpenda mtu italingana na moyo wako,je umeridhia kueka mtu kwa nafsi au la? Kuna wengi wamewahi kuwa kwa mapenzi na mwishowe kufurahia wengine kuumia mitimani mwao kiasi cha wengine kujitoa uhai.Unaweza kupenda au kupendwa na baadae ukatendwa huku ukiishia kujutia maishani,unabaki kusema tu 'laiti ningalijua'.
Mapenzi ni nini?Mapenzi ni idadi kadhaa ya hisia za ndani ,zisizoelezeka ,za kudumu kwa mtu mwingine,kuanzia mahaba ,pendo hadi upendo wa Kimungu. Kulingana na mada ya 'Haluwa si tamu tena vyuoni' ina maana kuwa mapenzi ya vyuoni yamechangia mambo mengi sana,mazuri na mabaya yake na yamekuwa kikwazo kwa baadhi ya wanagenzi. Mapenzi ya vyuoni yamezidi kushamiri sana kila uchao baina ya wanafunzi.Si Jambo la kutamausha kwani wakati mwingine pia utapata walimu wanaanzisha mahusiano na wanafunzi vyuoni.
Kuna mambo mengi sana ambayo yamechangiwa na mahusiano ya vyuoni dhidi ya wanafunzi.Kwanza kabisa,mapenzi ya vyuoni kati ya wanafunzi ni mazuri na kisha ni mabaya. Ukiangalia uzuri wa mapenzi ya vyuoni ni kuwa baada ya kuchumbiana kwa takribani miaka minne kwa kuvumiliana na kuaminiana, mwishowe kila mmoja anapata Kazi nzuri na kufunga pingu za maisha na baadae kuwa na maisha bora.Kutakuwa hakuna kudhaurauliana Kwa kuwa kila mmoja ako na kisomo chake ikizingatiwa kuwa siku za sasa ni kwamba ,bwana akileta kwa meza ,bibi na yeye afanye vivyo hivyo, hakuna ile kauli ya kusema 'mwanaume pochi mwanamke matumizi',kauli hiyo ilipitwa na wakati.
Mbali na hayo,kitu chochote kile kikiwa na uzuri ni lazima kama ibada kiwe na ubaya wake.Katika madhara ya mapenzi Kwa wanafunzi vyuoni ni; Mwanafunzi kukosa umakinifu anapokuwa chuoni, yaani anapoteza uwezo wa kutulia na kusikiliza mhadhiri darasani kwa sababu akili yake imejaa mambo chungu nzima.Pia kukosa uaminifu aidha kwa mwalimu au mzazi. Pindi anapojiingiza kwa mapenzi au mahusiano basi mwanafunzi yule atasalia kutumia lugha ya uongo kwa kuitisha fedha kutoka kwa mzazi wakati wowote ule kwa sababu anataka kumridhisha mpenzi wake.
Fauka ya hayo, mwanafunzi huanza tabia zisizoweza kurekebishika kamwe ,mfano hujiingiza katika michezo mibaya kama vile mchezo wa karata ili apate pesa ya kukidhi mahitaji ya mpenziwe.Mara zingine mwanagenzi hutumia njia mbadala faima ni kujiingiza wizi wa kimabavu ilimradi apate chochote kile cha kumfurahisha mpenziwe na hatimaye mwishowe anakumbana na mauti.
Pia idadi ya vifo kutokana na mapenzi ya vyuoni imeongezeka kwa asilimia kubwa sana.Kutokana na mawazo mengi yanayojaa akilini basi wanafunzi huchukua uamuzi wao mikononi na kufanya mambo ya kuasi.Ni mwaka jana tu ambapo visa vya wanafunzi wa vyuoni kujitia kitanzi wakiwa shuleni viliripotiwa.Haya yote chanzo chake ni mapenzi.Inauma na kukata maini kuona vijana wachanga mno ambao familia zao zinawategemea siku za usoni wakiangamia kwa kujitoa uhai.
Visa vya wanafunzi kupachikwa ujauzito wa mapema pia vimekithiri vyuoni.Utapata msichana anaripoti shuleni mwaka wa kwanza akiwa sawa ila ikifika muda wa likizo,anaporudi nyumbani hurudi akiwa na mtoto ama ujauzito uliosalia siku chache tu kujikopoa.Jamani tunaelekea wapi? Wazazi wanang'ang'ana kila uchao kumhakikishia mwanawe anapata mazingira mwafaka ya kusomea kwa kumlipia karo lakini mtoto anavalivalia miwani ya mbao swala la elimu na kujiingiza katika anasa huku akishikilia kikiki kauli ya kwamba,'ponda raha kufa kwaja'.Jambo la kuhuzunisha zaidi ni kwamba baadhi ya wanafunzi wa jinsia ya kike wanaavya ujauzito na kusalia kufukia viumbe huku wengine wakipoteza maisha kufuatia hatua hiyo.
Tunafaa kufahamu fika kuwa, kila kitu kina wakati wake.Pindi mtu anapopata nafasi ya kipekee ya kwenda chuo kikuu anafaa kushukuru Jaala Jalia pamoja na wazazi kwa jitihada walizofanya.Si rahisi kwa wazazi wengine kupeleka watoto wao vyuoni kwa sababu zisizoepukika.Ni lazima kwa wanafunzi kukumbatia elimu ili wajenge msingi mzuri wa maisha yao ya baadae, na kufahamu kuwa wazazi wanapitia hali ngumu ili wasije wakajutia kwani majuto ni mjukuu huja baadaye.
Kaz mbashara
ReplyDeleteKazi safi kaka
ReplyDeleteKazi nzuri kakangu
ReplyDelete๐
ReplyDeleteAwesome article
ReplyDeleteNoma
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDelete๐๐kazi nzuri
ReplyDeleteKuanzia mahaba hadi upendo
ReplyDeleteIla kama hilo pendo litakunyanyasa, litupilie mbali.
Kazi safi
Maneno kuntu๐
ReplyDeleteDats gud broo... kudos
ReplyDeleteInteresting article
ReplyDeleteKazi safi ๐ฅ
ReplyDeleteGood work
ReplyDeleteSure watu si wakuaminika
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteNakala Nzuri
ReplyDeleteKazi nzuri . Endelea hata na zaidi
ReplyDeleteKweli kabisa
ReplyDeleteGood ๐๐
ReplyDeleteKeep up the writing skills bro, good job for sure it will pay you one day
ReplyDeleteNice piece
ReplyDeleteSadakta
ReplyDeleteGood piece
ReplyDeleteKazi safi jomba
ReplyDeleteKazi Murua๐
ReplyDeleteGood job
ReplyDeleteSafi
ReplyDeleteKazi safi kiswaahili chenyewe Daaah
ReplyDeletePenda lakini upendo usikudidimize
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteMweledi wa hizi KAZI๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฏ
ReplyDeleteNice work
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteNakala nzuri.
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteAma kweli haluwa si tamu tena
ReplyDeleteKazi safiiiii
ReplyDeleteGreat article ๐
ReplyDeleteGood work somo
ReplyDeleteWow, congrats ๐๐๐
ReplyDeleteSwadakta
ReplyDeleteHongerea
ReplyDeleteKeep the fire burning...uko talented bro
ReplyDeleteKazi nzuri brother, keep it up
ReplyDeleteGood article ๐
ReplyDeleteKazi safi sana
ReplyDeleteGwiji
ReplyDeleteNice one
ReplyDeleteSwadaktumu
ReplyDeleteNyc
ReplyDeleteBin walah
ReplyDeleteGood work
ReplyDelete