MALEZI
UDONGO UWAHI UNGALI MAJI
Malezi
Malezi ni hali ya maandalizi ya mtoto kutoka utotoni hadi ukubwani ili kumwezesha kukua,kukubalika na kushiriki kwenye shughuli za kijamii kwa kumlinda na kumpatia mahitaji na huduma za kimsingi.
Kutokana na maana hiyo ya malezi ,basi ni sharti kama ibada ,kwa mzazi yeyote kuwa na mipango kabambe dhidi ya mtoto ili kufanikisha malezi murua.
Jambo la kutamausha katika Karne hii tunayoishi ni kwamba ,asilimia kubwa ya wazazi wameyaepuka majukumu yao na kusahau wajibu wao kwa watoto wao.Hali hii imechangiwa na mfumo wa kidijitali ambao umefanya wazazi wengi kuyaelekeza majukumu yao kwa wafanyikazi wa nyumba.
Siku hizi mzazi anathamini sana vifaa vya kielektroniki mfano simu hususan muda wa mapumziko baada ya kutoka kazini kuliko kukaa chini na mwanawe na kuzungumza mawili matatu.Hali yiyi hiyi ya kutotenga muda mwafaka wa kukaa na mtoto imezidi kuwa tumbo joto kwani visa vingi vya utomvu wa nidhamu miongoni mwa watoto vimekuwa vikishuhudiwa kila mara.
Ni mwaka jana tu ambapo visa chungu nzima vya wanafunzi kuteketeza mabweni shuleni na kufanya migomo ya mara kwa mara ,vilkuwa vikishamiri Kenya nzima huku maswali tata yakigonga vichwa vya habari ni nani wa kulaumiwa? Siku zote tunasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo ,pia ni dhahiri shahiri mahiri kuwa, nyumba huanza kwa msingi na mwalimu wa kwanza kabisa wa mtoto ni mzazi. Mzazi ana jukumu kubwa sana la kuhakikisha mwanawe anamkuza vyema kitabia. Kwa kawaida mtoto huanza kufunzwa nidhamu na mzaziwe akiwa nyumbani kabla ya kupelekwa shuleni, ni jambo la kustaajabisha kwa mtoto aliyelelewa malezi mema na ako na nidhamu ya hali ya juu kumwona akichukua hatua ya kuharibu mali ya shule.
Mighairi ya hayo,vijana wadogo ambao ni kioo na tegemeo la taifa la siku za usoni, siku hizi wamekuwa mstari wa mbele kufanya mashambulizi na kukabiliana ana kwa ana na polisi kwa sababu ya kutumia mihadarati na kujiunga na magenge ya wahalifu, hii yote inasababishwa na ukosefu wa malezi mema kutoka kwa mzazi.
Fauka ya hayo,visa ajira za mapema kwa watoto vinaongezeka kila uchao huku watoto hao wakinyanyaswa vikali na matajiri wao, hii yote imechangiwa na mzazi kutokuwa na muda maalum wa kuratibu na kumrudi vyema mwanawe na kumhakikishia usalama wa kutosha.
Kutokana na hali hiyo basi ,ni wajib na jukumu la kila mzazi kufahamu mtoto wake,atavaa nini atakula nini,atalala wapi, atasafiri vipi shuleni na atarudishwa na nani nyumbani.Haya yote mzazi akiyazingatia ,hatimaye mtoto atakuwa na maisha mema bila kikwazo chochote.
Kuntu wahenga waligonga ndipo waliposema , uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi na ni lazima kwa mzazi kuwa ange na kuhakikisha kuwa anamfanyia malezi mema mtoto katika kipindi chote cha maisha yake.
Hongera umeelezea kinagaubaga
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKazi nzuri🔥
ReplyDeleteWoooow. Kazi safi
ReplyDeleteKazi safi kaka
ReplyDeleteNdio maana nitazidi kumpa pongezi aliyekuwa Waziri wa elimu, Bw. Magoha kwa usemi wake kuwa mwanafunzi yoyote atakaye patikana na hatia ya uchamaji shule basi mzaziwe ndie atakaye gharamika.
ReplyDeleteNa si kwa hilo tu. Kuna mengi ameyafanya k.v kuja na mpango wa kusitisha usambazaji wa filamu za ngo** humu nchini.
Good work
ReplyDeleteSafi Kabisa Samaki Mkunje Angalia Mbichi
ReplyDeleteThis is a good piece bravo
ReplyDeleteKama wasemavyo wahenga samaki mkunje angali mbichi 💯
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteKazi nzuri kakaa
ReplyDeleteUmeua
ReplyDeleteKazi njema hongera!!
ReplyDeleteKweli kabisa
ReplyDeleteKazi safi 🔥
ReplyDeleteNakala nzuri
ReplyDeleteInahusunisha sana kupata wazazi wadogo kwenye ndoa wakikimbia majukumu yao.Naona Ndoa yataka mafunzo kabla ya kuchukua hatua ya kuwa wachumba.
ReplyDeleteKazi nzuri kaka
ReplyDeleteNakala nzuri sana kaka🔥
ReplyDeleteKweli💯
ReplyDeleteHongera 🔥
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteHongera kaka
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteKazi safi👏👌
ReplyDeleteHeko
ReplyDeleteKazi.safi
ReplyDeleteKazi nzuri sana
ReplyDeleteSadakta
ReplyDeleteNa Basi CBC ihalalishwe shuleni kwa sababu mafunzo yake yawafanya watoto kukuwa na Tabia fulani ya kinidhamu
ReplyDeleteWahuni si watu wazuri😂
ReplyDelete👏👏
ReplyDeleteGood work. Keep it up my brother you are capable of. Excellent.
ReplyDeleteDeal well done. Congrats bro.
ReplyDeleteGreat content
ReplyDeleteGood work brooo
ReplyDeleteExplicit
ReplyDeleteKazi nzuriii
ReplyDeleteNice one bro
ReplyDeleteKazi nzuri kaka
ReplyDeleteGood job bro
ReplyDeleteGood work
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteNice
ReplyDelete