BAADA YA DHIKI FARAJA

 Babu yangu,Mzee Abdhalah angefufuka leo kisha aone vile halaiki ya watu wanavyoumia kutokana na gharama ya juu ya maisha, angeanguka na kuzimia.Atakapozinduka angemwomba Maulana amrudishe katika kaburi lake huko Kilifi au angekubali mwenyewe kuendelea kuishi ili ajionee masaibu yanayowakumba wajukuu wake kutokana na garama ya uchumi.

Baada ya wakazi wa Kaunti ya Mombasa kuteseka kwa miaka na mikaka kufuatia kuhamishwa kwa  huduma za mamlaka ya bandari  Nchini Kenya na kupelekwa Kaunti ya Naivasha,sasa ni afueni kwao kwani hatimaye baada ya kuapishwa kwa Rais wa taifa William Samoei Ruto,aliamuru mara moja kurejeshwa kwa huduma za bandari mjini Mombasa. 

Je,kuna manufaa yoyote kwa wakazi wa Kaunti ya Mombasa kwa kurudishwa kwa huduma za bandari? Wahedi,ni tabasamu sasa kwa wakazi wote wa pwani kwani nafasi za ajira zitajaa pomoni huku waliokosa vibarua kwa muda mwingi watapata nafasi nzuri ya kufanya kazi bandarini.Fauka ya hayo,idadi ya vijana ambao wamejiingiza kwenye  uraibu wa kutumia mihadarati hatimaye itapungua kwa asilimia kubwa.Vijana wengi watanufaika na kujitoa katika limbi la umaskini ambao umewavamia kama nzige kwenye shamba la mahindi na kujikimu kimaisha.

Pia kurudishwa kwa huduma za bandari kutasaidia uchumi wa taifa la Kenya kuimarika kwa kiwango kikubwa,kwani watu wengi wataekeza kutokana na mishahara yao kisha baadae kujifungulia biashara zao binafsi.

Pia wafanyibiashara wadogo wadogo kama vile mama mboga,bodaboda na hata wauzaji vyakula vibandani, biashara zao zitaimarika vizuri kwani wenye kufanya kazi bandarini, watategemea huduma za wafanyibiashara hawa kwa kiasi kikubwa mno.Vilevile idadi ya visa na magenge ya uhalifu kama vile wakali kwanza,yatapungua kwani vijana wengi watajihusisha na kazi pasi mzaha ikizingatiwa kuwa baadhi ya  magenge hayo ni vijana tu wanaozurura mtaani na kuhangaisha wenyeji.

Kaditama ni kwamba mji wa Mombasa utakuwa na haiba ya kipekee na kuchukua sura mpya kuliko ulivyo sasa.Sote tunajua fika kuwa Kaunti ya Mombasa imetambulika sana kwa visa vya utomvu wa nidhamu hadi ikapelekea kuongezwa kwa idadi ya Askari ili usalama uimarike.Sasa itakuwa hali ya usalama Mombasani itakuwa shwari kwa kuwa vijana wengi watakuwa wakifanya kazi bandarini na kuepeka visa vya kupora vibeti na kulaghai watu kila kona ya mji huu.



Comments

  1. Kazi kuntu๐Ÿ‘Œkeep the ๐Ÿ”ฅ burning

    ReplyDelete
  2. ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

    ReplyDelete
  3. Mjukuu wa babu abdallah nakupa hongera.. utunzi mzuri

    ReplyDelete
  4. ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ’ฏ

    ReplyDelete
  5. Mashallah ๐Ÿ’ฅ๐Ÿ’ฅ๐Ÿ™Œ

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

HALUWA SI TAMU TENA VYUONI

MALEZI