BAADA YA DHIKI FARAJA
Babu yangu,Mzee Abdhalah angefufuka leo kisha aone vile halaiki ya watu wanavyoumia kutokana na gharama ya juu ya maisha, angeanguka na kuzimia.Atakapozinduka angemwomba Maulana amrudishe katika kaburi lake huko Kilifi au angekubali mwenyewe kuendelea kuishi ili ajionee masaibu yanayowakumba wajukuu wake kutokana na garama ya uchumi.
Baada ya wakazi wa Kaunti ya Mombasa kuteseka kwa miaka na mikaka kufuatia kuhamishwa kwa huduma za mamlaka ya bandari Nchini Kenya na kupelekwa Kaunti ya Naivasha,sasa ni afueni kwao kwani hatimaye baada ya kuapishwa kwa Rais wa taifa William Samoei Ruto,aliamuru mara moja kurejeshwa kwa huduma za bandari mjini Mombasa.
Je,kuna manufaa yoyote kwa wakazi wa Kaunti ya Mombasa kwa kurudishwa kwa huduma za bandari? Wahedi,ni tabasamu sasa kwa wakazi wote wa pwani kwani nafasi za ajira zitajaa pomoni huku waliokosa vibarua kwa muda mwingi watapata nafasi nzuri ya kufanya kazi bandarini.Fauka ya hayo,idadi ya vijana ambao wamejiingiza kwenye uraibu wa kutumia mihadarati hatimaye itapungua kwa asilimia kubwa.Vijana wengi watanufaika na kujitoa katika limbi la umaskini ambao umewavamia kama nzige kwenye shamba la mahindi na kujikimu kimaisha.
Pia kurudishwa kwa huduma za bandari kutasaidia uchumi wa taifa la Kenya kuimarika kwa kiwango kikubwa,kwani watu wengi wataekeza kutokana na mishahara yao kisha baadae kujifungulia biashara zao binafsi.
Pia wafanyibiashara wadogo wadogo kama vile mama mboga,bodaboda na hata wauzaji vyakula vibandani, biashara zao zitaimarika vizuri kwani wenye kufanya kazi bandarini, watategemea huduma za wafanyibiashara hawa kwa kiasi kikubwa mno.Vilevile idadi ya visa na magenge ya uhalifu kama vile wakali kwanza,yatapungua kwani vijana wengi watajihusisha na kazi pasi mzaha ikizingatiwa kuwa baadhi ya magenge hayo ni vijana tu wanaozurura mtaani na kuhangaisha wenyeji.
Kaditama ni kwamba mji wa Mombasa utakuwa na haiba ya kipekee na kuchukua sura mpya kuliko ulivyo sasa.Sote tunajua fika kuwa Kaunti ya Mombasa imetambulika sana kwa visa vya utomvu wa nidhamu hadi ikapelekea kuongezwa kwa idadi ya Askari ili usalama uimarike.Sasa itakuwa hali ya usalama Mombasani itakuwa shwari kwa kuwa vijana wengi watakuwa wakifanya kazi bandarini na kuepeka visa vya kupora vibeti na kulaghai watu kila kona ya mji huu.
Kazi murua kabsa...
ReplyDeleteheko
ReplyDeleteKazi safiii
ReplyDeleteKweli kaka umenena๐ช
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteGood work
ReplyDelete๐ฅ๐ฅ๐ฏ
ReplyDeleteKunthuuuu
ReplyDeleteMakala mazuri haya
ReplyDeleteKazi safi bro
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteSwadakta mkuu
ReplyDeleteKweli kabisa
ReplyDeleteKazi nzuri sana kaka
Kazi nzuri
ReplyDeleteKazi kuntu๐keep the ๐ฅ burning
ReplyDeleteFaraja kwa kweli
ReplyDeleteKazi kuntu
ReplyDelete๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
ReplyDeleteKazi kali kaka๐
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteMjukuu wa babu abdallah nakupa hongera.. utunzi mzuri
ReplyDeleteKweli kabisa
ReplyDeleteKizazi sana
ReplyDeleteSanaa imeweza
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteNice work
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKazi Nzuri ๐
ReplyDeleteNice one
ReplyDelete๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฏ
ReplyDeleteGood job
ReplyDeleteGood job
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteNice work
ReplyDeleteMashallah ๐ฅ๐ฅ๐
ReplyDeleteKazi safi ndugu๐
ReplyDeleteGood job
ReplyDelete