MACHO YOTE SASA YAELEKEZWA KWA VIJANA KATIKA KUFUFUA UCHUMI WA TAIFA


               Picha angavu kwa hisani ya Google

Je, vijana wana umuhimu wowote katika kufufua uchumi wa Kenya? Hilo ndilo swali ambalo linazidi kuumiza mishipa vichwani mwa waja wengi katika siku za hivi sasa.Hali ya uchumi imeenda juu kiasi kwamba imekuwa donda sugu lisilopona.Mamia ya waja wanazidi kupoteza maisha yao kila uchao kutokana na njaa ambayo imesababishwa na gharama ya juu ya maisha.Familia nyingi haziwezi kujimudu tena sikwambii kutosheleza mahitaji yao ya kimsingi.Habari zinazongonga vichwa vya wanahabari kila uchao ni kwamba suluhu itapatikana wapi ili kuokoa maisha ya binadamu?Wanahabari kote nchini wapo ange kuhakikisha kuwa wanataoa taarifa kemkem kuhusu familia zilizoathirika kutokana na kupanda kwa uchumi hapa nchini.Ni lazima kama ibada kuwa kilicho na sifa acha kipewe sifa, hii ni kumaanisha kuwa hongera kwa wanahabari wetu waliosimama kidete na kuangazia masaibu ya waja wanayopitia,ni kutokana na bidii zao za kuripoti ndiposa wahisani kutoka kila pembe ya nchi wamejitokeza waziwazi kama jino la ngiri na kusaidia waathirika.

Hayo yote tisa, kumi ni kuwa vijana pia wana uwezo mkubwa katika kurudisha sura mpya ya taifa la Kenya jinsi lilivyokuwa hapo awali.Kusema kweli hali ilivyo sasa inahuzunisha na kustaajabisha mno.Bei za bidhaa muhimu ziko juu kama bendera lakini matumaini yangalipo kwani vijana wako mbioni kuhakikisha kila kitu kinarudi pahali pake.Kwanza kabisa vijana wako mbioni kutafuta vibaraua ili kukidhi mahitaji ya yao ya kimsingi, ni kupitia ajira hizo ndio uchumi wa taifa letu utafufuka.Hongera kwa serikali kwa kuwa na mpango wa kupatia vijana mtaji ili waanzishe biashara.

Fauka ya hayo,vijana wanapojihusisha na ajira bila shaka watalipa ushuru kama ilivyo ada na desturi katika taifa letu tukufu la Kenya, kutokana na hiyo pesa ya ushuru ndipo serikali itaweza kupanga mipango kabambe ya kuamsha hali ya uchumi iliyolala fofofo.Pia vijana watafufua uchumi wa taifa pindi watakapojihusisha na mambo na kilimo ikizingatiwa kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa Kenya.Vijana endapo watajitolea asilimia mia kwa mia na kuzamia kilimo basi nchi yetu itaweza kuzalisha chakula kwa wingi na janga hili la njaa tutalizika katika kaburi la sahau.Tukizingatia kilimo basi taifa hili litaweza kutosheleza waja wake na hata kuuza bidhaa zetu mataifa ya nje na hapo ndipo tutapata pesa zaidi ya kustawisha Kenya yetu.Vijana tusilalie masikio tujitume katika ukulima ili tuweze kujitegemea wenyewe siku za usoni.Pia tukiweza kujitegemea serikali yetu itapumua katika kuomba mikopo kutoka mataifa mengine.


                 Picha ngavu kwa hisani ya google

 Mbali na hayo ni kwamba kubuniwa kwa nafasi za kazi kwa vijana na serikali za kaunti na kitaifa kutawezesha vijana kuinua uchumi wa taifa uliodorora kwa siku nyingi.Vile vile vijana wanao uwezo wa wao binafsi kujifungulia biashara na hali hii itachangia kurudisha hali ya uchumi ilivyokuwa hapo awali.Pindi vijana wanapojiingiza kazini basi visa vya utovu wa usalama pia vitapungua mara dufu.Hali ya usalama itarudi kama kawa kama dawa kwa sababu kila mmoja atakuwa anatosheka na pato lake.Hata hivyo pindi vijana watakaporudisha hali ya uchumi pahali pake basi wageni wengi watazuru taifa letu na kutokana na hilo tutapata pesa za kigeni ambazo zitatumika katika kueka muonekano mpya wa taifa letu.Kilicho na mwanzo hakikosi mwisho,wito kwa serikali yetu ya kitaifa kuhakikisha swala la ajira kwa vijana inalipa kipaumbele kwani vijana ndio kioo cha jamii.Vijana kama ilivyo ada na desturi kuwa nyinyi ndio tegemeo la siku za usoni basi hatuna budi kung’ang’ana kama mchwa kichuguuni ili kuboresha na kurudisha hali ya uchumi wa taifa la Kenya mahali ulipokuwa.

 

Mwandishi wa Makala haya ni Mohammed Kazungu kutoka Chuo kikuu cha Kiufundi cha Mombasa (TUM)

 

Comments

  1. Huu ndio Wimbo kila sehemu ya Dunia.Jitahidi sana kujiajiri tuepuke hili

    ReplyDelete
  2. Nice and good

    ReplyDelete
  3. Kazi nzuri 👏👏

    ReplyDelete
  4. Uko juu brother nice one

    ReplyDelete
  5. Another beautiful narration, keep it up buddy

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

HALUWA SI TAMU TENA VYUONI

MALEZI

BAADA YA DHIKI FARAJA